Posts

Showing posts from August 2, 2026

Submission si Obedience: Je, Biblia Inafundisha Nini Kuhusu Wajibu wa Mume na Mke?

Image
  Submission si Obedience: Je, Biblia Inafundisha Nini Kuhusu Wajibu wa Mume na Mke? Na Ipyana Amon Mwakosya Moja ya mafundisho yanayojadiliwa sana katika Ukristo ni uhusiano kati ya mume na mke, hasa kuhusu maneno "submission" (kujitiisha) na "obedience" (kutii) . Watu wengi huyachukulia maneno haya kuwa na maana moja, lakini Biblia inatumia maneno tofauti. Je, tofauti hiyo ina maana gani? 1. Mume ni nani? Kwa lugha ya Kigiriki ya Agano Jipya, neno linalotafsiriwa mume ni ἀνήρ ( anēr ) , ambalo maana yake ya msingi ni mwanaume mzima . Linapotumika katika muktadha wa ndoa, hutafsiriwa mume . Hii inaonyesha kwamba neno "mume" halimaanishi mtu anayewatawala wengine, bali mwanaume aliye katika agano la ndoa. Kwa upande wa Kiingereza, neno husband limetokana na Old Norse húsbóndi , lililomaanisha mwenye kaya au msimamizi wa nyumba . Hata hivyo, etimolojia ya neno la Kiingereza haipaswi kuchukuliwa kama tafsiri ya moja kwa moja ya maneno ya Biblia, ambayo y...