Submission si Obedience: Je, Biblia Inafundisha Nini Kuhusu Wajibu wa Mume na Mke?

 

Submission si Obedience: Je, Biblia Inafundisha Nini Kuhusu Wajibu wa Mume na Mke?

Na Ipyana Amon Mwakosya

Moja ya mafundisho yanayojadiliwa sana katika Ukristo ni uhusiano kati ya mume na mke, hasa kuhusu maneno "submission" (kujitiisha) na "obedience" (kutii). Watu wengi huyachukulia maneno haya kuwa na maana moja, lakini Biblia inatumia maneno tofauti. Je, tofauti hiyo ina maana gani?

1. Mume ni nani?

Kwa lugha ya Kigiriki ya Agano Jipya, neno linalotafsiriwa mume ni ἀνήρ (anēr), ambalo maana yake ya msingi ni mwanaume mzima. Linapotumika katika muktadha wa ndoa, hutafsiriwa mume.

Hii inaonyesha kwamba neno "mume" halimaanishi mtu anayewatawala wengine, bali mwanaume aliye katika agano la ndoa.

Kwa upande wa Kiingereza, neno husband limetokana na Old Norse húsbóndi, lililomaanisha mwenye kaya au msimamizi wa nyumba. Hata hivyo, etimolojia ya neno la Kiingereza haipaswi kuchukuliwa kama tafsiri ya moja kwa moja ya maneno ya Biblia, ambayo yaliandikwa kwa Kigiriki.

2. Kwa nini Biblia haisemi "Wake, watiini waume zenu"?

Biblia ya Kiswahili imetumia neno watiifu (obey) lakini biblia ya kigiriki na kingereza zimetumia neno Submissive (kujitiisha). Neno obey na neno Submissive zinautofauti japo kwenye biblia ya hawajatofautisha. Ila kwenye hili somo nitazitofautisha kwa lengo la kupata maana sahihi iliyokusudiwa na mwandishi husika

Katika Waefeso 5:22, Paulo anaandika:

"Wake, wajitiishe (submissive ) kwa waume zenu kama kwa Bwana."

Neno lililotumika hapa si ὑπακούω (hypakouō), ambalo humaanisha kutii amri, bali ni ὑποτάσσω (hypotassō), ambalo humaanisha kujipanga chini ya uongozi au utaratibu kwa hiari.

Paulo anatumia hypakouō kwa watoto:

"Enyi watoto, watiini wazazi wenu..." (Waefeso 6:1)

Na pia kwa watumwa:

"Enyi watumwa, watiini mabwana zenu..." (Waefeso 6:5)

Lakini kwa wake, anatumia hypotassō.

Hii inaonyesha kwamba Paulo alitofautisha uhusiano wa ndoa na uhusiano wa mzazi na mtoto au bwana na mtumwa.

3. Je, Submission ni Automatic?

Hapana.

Submission si kitendo kinachotokea bila uchaguzi wa mtu. Ni uamuzi wa moyo unaofanywa kwa hiari mbele za Mungu.

Vivyo hivyo, Biblia haisemi kwamba mume anaweza kumlazimisha mke kuwa submissive. Wame wengi huzani mwanamke anaweza kuwa submissive kwake kiurahisi lakini sio wala sio ngumu ila inawezekana kufanyika kwa kumtegemea Mungu.

4. Je, Mume Anaweza Kumfanya Mke Awe Submissive?

Biblia haimpi mume amri ya:

"Wafanyeni wake zenu wajitiishe (submissive)."

Badala yake inasema:

"Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake." (Waefeso 5:25)

Kristo hakulazimisha kanisa limfuate. Aliwashinda watu kwa:

  • upendo,

  • kujitoa,

  • ukweli,

  • na utakatifu.

Huo ndio mfano ambao waume wamepewa.

5. Ni Nini Hujenga Submission?

Hakuna mbinu ya kumlazimisha mtu awe submissive. Lakini kuna tabia zinazojenga mazingira ya kuaminiana:

  • Upendo wa kweli.

  • Uaminifu.

  • Hekima katika maamuzi.

  • Uwajibikaji.

  • Kujitoa kwa familia.

  • Unyenyekevu.

  • Maisha yanayofanana na ya Kristo.

Mke anapomwona mume wake akiishi kwa namna hiyo, uaminifu na heshima huongezeka. Hata hivyo, submission bado ni uchaguzi wa mke mbele za Mungu.

6. Mamlaka Huambatana na Wajibu

Biblia inasema:

"Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa." (Waefeso 5:23)

Lakini mara moja Paulo anaeleza aina ya uongozi anaouzungumzia:

"Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa."

Kwa hiyo mamlaka ya mume si ruhusa ya kutawala kwa mabavu, bali ni wito wa:

  • kupenda,

  • kulinda,

  • kuhudumia,

  • na kujitoa.

Kadiri mamlaka yanavyoongezeka, ndivyo wajibu unavyoongezeka.

Hivyo Basi.

Biblia haifundishi kwamba mke ni mtumwa wa mume, wala haifundishi kwamba mume anapaswa kutawala kwa nguvu.

Badala yake, inafundisha kwamba:

  • mume aishi kwa mfano wa Kristo,

  • mke ajitiishe kwa hiari kwa utaratibu wa Mungu,

  • na wote wawili waishi katika upendo, heshima, na kujitoa kwa kila mmoja.

Submission ya kweli haiwezi kuzalishwa kwa hofu au kulazimishwa. Hukua pale ambapo upendo wa Kristo unaonekana katika maisha ya mume, na mke anachagua kuitikia wito wa Mungu kwa moyo wa hiari.

"Mume hawezi kuamuru submission; anaalikwa kuishi maisha yanayostahili kuaminika. Na mke haamriwi kuwa mtumwa, bali anaitwa kujitiisha kwa hiari katika mpango wa Mungu wa ndoa."

Mungu aiimarishe ndoa zetu kwa upendo, ukweli, na neema yake. Amen.



Comments

Popular posts from this blog

Activate the Mind of Christ in You

Does God Choose to Love?

God's Constant & Equal Love